Rais William Ruto mapema leo Alhamisi katika Ikulu ya Nairobi, amepokea hati za Mabalozi watatu waliotumwa kuhudumu humu nchini.
Mabalozi hao ni Rulan Mahmoud Samara wa Jordan, Jacinto Januario Maguni kutoka Msumbiji na Saad Bin Abdullah AlNofaia kutoka Saudi Arabia.
Rais Ruto amewahakikishia kuwa atawaunga mkono katika utenda kazi wao kwa kipindi watakachohudumu nchini.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Rais Ruto aidha alisema taifa hili linaimarisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi duniani kote.
Amesema lengo la hatua hiyo ni kuboresha ushirikiano na nchi hizo na hivyo kufungua milango ya fursa mpya kwa manufaa ya pande zote mbili.