Walioshambuliwa na wanyamapori wapokea ridhaa ya shilingi milioni 950

Dismas Otuke
0 Min Read

Shirika la Wanyamapori nchini (KWS) limetoa ridhaa ya shilingi milioni 950 kwa waathiriwa wa mashambulizi ya wanyamapori humu nchini.

Akiongoza hafla hiyo jana Jumatano, Kamishna wa kaunti ya Meru Jacob Ouma aliwataka waathiriwa wote kuwa waaminifu  wanapowasilisha malalamishi yao ya visa vya kushambuliwa na wanyamapori.

Aidha, alifichua kuwa KWS inapanga kukita ua wa umeme wa umbali wa kilomita 42 ili kupunguza mizozo ya wanyamapori na binadamu.

TAGGED:
Share This Article