Kodak Black akosa kufika kwenye tamasha lake Texas

Dismas Otuke
1 Min Read

Msanii wa muziki nchini Marekani Kodak Black alikosa kufika kwenye tamasha lake huko Midland, Texas nchini Marekani.

Tamasha hilo lilikuwa limepangiwa kuandaliwa Ijumaa Februari 27, 2026 lakini haikuwezekana kutokana na kile ambacho usimamizi wake unakitaja kuwa kucheleweshwa kwa safari yake ya ndege.

Wakili wa Kodak aitwaye Bradford Cohen alielezea kwamba kutupiliwa mbali kwa tamasha hilo hakukutokana na utepetevu wa msanii huyo bali kulitokana na shida za usafiri.

Kulingana na Cohen, Kodak alifaa kuondoka Florida kuelekea Texas kwa ndege lakini mmiliki wa ndege ambayo ingembeba akabadili mipango dakika za mwisho mwisho.

Kodak aliwasiliana na mmiliki huyo ambaye alimpa ndege nyingine lakini katika uwanja tofauti wa ndege na walipofika eneo la Tamasha walipata kumefungwa.

Wakili Cohen anasema Kodak alihuzunika sana kwa kukosea mashabiki waliokuwa wamenunua tiketi za tamasha hilo ndiposa akaingia katika eneo jingine huko huko Midland akatumbuiza bure bila malipo.

Usimamizi wa eneo alilokuwa amepanga kuandaa tamasha lake ulitoa taarifa ukiomba mashabiki msamaha na kuwahimiza kuomba kurejeshewa pesa zao iwapo wangetaka.

Share This Article