Rooney Onyango afungiwa kucheza na ADAK

Dismas Otuke
1 Min Read

Beki wa Harambee Stars Rooney Onyango amefungiwa kushiriki soka baada ya kupatikana na hatia ya kukwepa vipimo dhidi ya ulaji muku.

Shirika la kupambana na ulaji muku ADAK, limesema kuwa Onyango, alikosa kuwaelezea maafisa wake alipokuwa mara mbili ndani ya miezi 12 na pia kukosa vipimo vya ulaji muku mara moja.

Kwa jumla Onyango ambaye zamani alikuwa akiichezea Gor Mahia, kabla ya kuhamia klabu ya Sognadal ya Norway alikosa vipimo vya ulaji muku mara tatu ndani ya kipindi cha miezi 12.

Share This Article