Rais wa Cameroon mwenye umri wa miaka 92, Paul Biya, ameapishwa kwa muhula mwingine wa miaka saba katika hafla iliyoandaliwa bungeni mjini Yaoundé.
Biya ambaye ndiye Rais mkongwe zaidi duniani, alipata ushindi wa muhula wa nane, ingawa uchaguzi huo ulizua utata mkubwa mwezi Oktoba.
Rais huyo ameiongoza nchi hiyo kwa miaka 43, na kabla ya uchaguzi huo, alihudhuria mkutano mmoja tu wa kampeni.
Rais huyo ambaye ndiye rais mkongwe zaidi duniani, alishinda kwa asilimia 54 ya kura ikilinganishwa na asilimia 35 za kura za mpinzani wake wa karibu Issa Tchiroma Bakary, kwa mujibu wa matokeo rasmi.
Tchiroma Bakary amesisitiza kuwa yeye ndiye aliyekuwa mshindi sahihi wa uchaguzi huo na ameshutumu maafisa husika kwa ulaghai ambao wamekanusha.
Matokeo ya uchaguzi huo yalipotangazwa maandamano yalizuka kote nchini.