Kamati ya Ulinzi Bungeni yaahidi kuongeza mgao wa bajeti kwa jeshi la wanamaji

Dismas Otuke
1 Min Read

Kamati ya ulinzi katika bunge la kitaifa imeahidi kuongeza mgao wa bajeti kwa jeshi la wanamaji nchini.

Kamati hiyo imesema haya Ijumaa lilipokagua kituo cha wanajeshi wa majini eneo la Malindi.

Ikiongozwa na naibu mwenyekiti Bashir Abdullahi, kamati hiyo ilikutana na Luteni Kanali James Munyao, anayesimamia kituo hicho katika juhudi za kuangalia miundombinu na vifaa vya wanajeshi wa majini.

Kamati hiyo hata hivyo imehoji vifaa vya kupiga doria vilivyochakaa na kupendekeza kununuliwa kwa vifaa vipya.

Share This Article