Tanzania kurejea kwa Mkapa wakiwinda ushindi wa pili leo dhidi ya Mauritania

Taifa Stars watashuka uwanjani wakilenga ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kwa robo fainali

Dismas Otuke
1 Min Read

Wenyeji wenza wa michuano ya CHAN, Tanzania, ukipenda Taifa Stars, watarejea katika uwanja wa kitaifa wa Benjamin Mkapa leo Jumatano usiku kwa mchuano wa pili wa kundi B dhidi ya Mauritania.

Taifa Stars watashuka uwanjani wakilenga ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kwa robo fainali kwa mara ya kwanza, baada ya kuishinda Burkina Faso 2-0 katika pambano la ufunguzi.

Mechi hiyo itang’oa nanga saa mbili usiku, na itatanguliwa na ile kati ya Afrika ya Kati dhidi ya Burkina Faso saa kumi na moja.

Burkina Faso – The Stallions watalenga ushindi ili kusalia mashindanoni baada ya kupoteza mechi ya ufunguzi.

Upande mwingine Afrika ya kati itakuwa ikicheza mechi ya kwanza .

Share This Article