30 ya Bongo Fleva yaelekea Mwanza

Awamu ya kwanza ya tamasha hiyo ilifanyika Julai 10, 2026, ndani ya Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Marion Bosire
1 Min Read

Sherehe ya miaka 30 ya muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania sasa inaelekea katika mkoa wa Mwanza.

Tamasha hiyo itaandaliwa Agosti 8, 2026 katika eneo la burudani la The Climax, ndani ya jumba la kibiashara la Rock City ambapo wasanii kama Ay, Q Chief, 20 Percent, Juma Nature, Ferooz na King GK watatumbuiza.

Hao ni baadhi tu ya wanamuziki ambao vipaji vyao vimeelekeza tasnia ya Bongo fleva na kuipa heshima ambayo leo hii imezalisha ajira na maisha kwa vipaji vingine vingi nchini Tanzania.

Tamasha za kusherehekea miaka 30 ya Bongo Fleva zinatarajiwa kuandaliwa katika maeneo mbali mbali nchini Tanzania baada ya hafla kubwa ya uzinduzi iliyofanyika Julai 10, 2026, ndani ya Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Ni katika uzinduzi huo waandalizi walitangaza kwamba tamasha nyingine zitaandaliwa nje ya Dar es Salaam.

Share This Article