Zaidi ya watu laki mbili wamefurushwa makwao katika eno Kordofan nchini Sudan kutokana na mapigano yaliyozuka mwaka jana.
Kwa mjibu wa Umoja wa Mataifa vita ambavyo vimekuwa vikiendelea tangu mwaka jana kupitia kwa droni na mashambulizi ya angani vimeathiri miundo mbinu muhimu ikiwemo umeme na maji katika mji wa El Obeid .
Umoja wa Mataifa umeongeza kuwa mafuriko yaliyoshudiwa katika eneo lililo karibu la Dar Fur kaskazini yamefanya hali kuwa tete zaidi.
Aidha, mapigano makali yameshuhudiwa eneo la El Obeid pia yamesababisha kutoweka kwa umeme na kukatizwa kwa maji misongamao mikubwa hospitalini na hata kukatiza mawasiliano ya simu.
Katika eneo la Blue Nile watu wapatao 78,000 wamekimbia makwao huku 18,000, wakitoroka eneo la magharibi mwa Darfur katika nusu ya kwanza ya mwezi huu wa Agosti.
Wakati ou huo mvua kubwa iliyonyesha kaskazini mwa Darfur naa eneo la Tawila imeaharibu nyumba zipatazo 1,350, huku familia zaidi ya 1,000 zikiachwa bila makao.