Kiongozi wa chama cha ODM, Seneta Oburu Oginga, ametoa onyo kali kwa wale wote wenye lengo la kukigawanya chama akiwataka wote wasioridhika waondoke.
Akizungumza kwenye mkutano wa kisiasa ujulikanao kama Linda Ground katika kaunti ya Siaya, Oburu amesisitiza kuwa chama hicho kwa sasa kinafanya mashauriano ya kisera, miradi ya maendeleo na pia ugavi wa mamlaka kuelekea katuka uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.
Aidha Oburu amesema kuwa chama cha ODM, kimekuwa kwenye upinzani kwa muda mrefu zaidi na yuko tayari kuhakikisha kuwa kitakuwa ndani ya serikali ijayo.