Serikali kuanza kuwafurusha Wafanyabiashara wa kigeni na wachuuzi wasio na leseni kuanzia wiki ijayo

Aidha,aliwataka maafisa wa Serikali kutathmini na kurekebisha  misingi ya kutoa leseni kwa wafanyabiashara wa kigeni humu nchini.

Dismas Otuke
1 Min Read

Serikali imetangaza kuanza msako wa kukabiliana na Wafanyabiashara  wa kigeni na wachuuzi wasio na leseni kuanzia Septemba 7.

Akitangaza hatua hiyo  Jumatano jioni katika Ikulu ya Nairobi alipokutana na waekezaji,Rais Ruto alisema ni jukumu la serikali kuwalinda wafanyabiashara dhidi ya ushindani usio halali.

Rais aliongeza  tayari mswada uko bungeni ambao ukipitishwa utazuaia raia wa kigeni kufanya  biashara fulani zinazostahili kufanywa na Wakenya pekee.

Aidha,aliwataka maafisa wa Serikali kutathmini na kurekebisha  misingi ya kutoa leseni kwa wafanyabiashara wa kigeni humu nchini.

 

Share This Article