Roast and Rhyme: Wasanii watakaotumbuiza watajwa

Cindy Sanyu, Fik Fameica na Dax Vibez wamethibitishwa kutumbuiza katika maadhimisho hayo ya miaka 10 ya tamasha hiyo.

Marion Bosire
1 Min Read
Cindy Sanyu

Tarehe ya siku ya tamasha maarufu ya Roast and Rhyme nchini Uganda inazidi kusogea karibu  huku waandalizi wakitaja wasanii wakuu watakaotumbuiza kwenye awamu hiyo ya 10.

Wasanii wa Uganda Cindy Sanyu, Fik Fameica na Dax Vibez wamethibitishwa kutumbuiza katika maadhimisho hayo ya miaka 10 ya tamasha ya Roast And Rhyme, itakayofanyika Jumapili, Desemba 6, 2026, katika uwanja wa mchezo wa magongo yaani Hockey, huko Lugogo, jijini Kampala.

Wasanii hao watakuwa kivutio kikuu cha tamasha hiyo wakiongozana na bendi ya Ivuga na Double Black katika kusherehekea mwongo mmoja wa tamasha hiyo maarufu ya burudani ya nje.

Tamasha hiyo ambayo huandaliwa na kampuni ya Swangz Avenue itajumuisha muziki wa moja kwa moja, nyama choma na burudani mbalimbali, huku mashabiki wakitarajiwa kufurahia siku nzima ya maonyesho na sherehe.

Kwa miaka mingi, Roast And Rhyme imekua na kuwa moja ya matukio maarufu katika kalenda ya burudani nchini Uganda, ikivutia familia, marafiki na wapenzi wa muziki wanaofurahia chakula, burudani na mazingira ya wazi.

Itaanza saa 5 asubuhi, huku waandaaji wakihimiza mashabiki kufika mapema ili kufurahia shughuli za siku nzima.

hafla hiyo itakuwa fursa ya kuadhimisha safari ya miaka 10 ya tamasha hiyo pamoja na mashabiki, wasanii na washirika waliochangia ukuaji wake.

Share This Article