Mwanafunzi awapiga risasi watu sita Marekani

Tom Mathinji
1 Min Read

Mwanafunzi mmoja amewapiga risasi watu sita, na kuuwa mmoja katika shule ya sekondari katika jimbo la Iowa nchini Marekani, na kisha kujitoa uhai.

Tukio hilo limetokea siku ya kwanza wanafunzi waliporudi shule baada ya mapumziko ya likizo, polisi wamesema.

Watano kati ya waliopigwa risasi walikuwa ni wanafunzi na mmoja ni msimamizi wa shule.

Mwanafunzi aliyefariki alikuwa darasa la sita, ambalo ni la watoto wa miaka 11 au 12.

Mshukiwa huyo baadaye alitambuliwa kama Dylan Butler, alikuwa mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17.

TAGGED:
Share This Article