Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda siku ya Ijumaa ameupokea rasmi mwili wa aliyekuwa Mfalme wa Tooro, Oyo Nyimba Kabamba Iguru Rukidi wa nne katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Entebe.
Ndege iliyobeba mwili wa marehemu Mfalme Oyo, ilitua muda mfupi kabla ya saa saba kutokea texas, Marekani alikofia akipokea matibabu.
Museveni aliweka shada la maua juu ya jeneza la marehemu na baadaye kuzugumza jinsi walivyokutana mwaka jana ambapo aliahidi kugharimia matibabu yake Ujerumani na baadaye nchini Marekani.
Mfalme Oyo aliyefariki kutokana na saratani akiwa na umri wa miaka 35 atazikwa Septemba 12.
Punde baada ya hafla hiyo ya kuupokea mwili, mwili uliwekwa katika ndege ya kijeshi na kusafirishwa hadi Tooro.