KQ yanakili hasara ya shilingi bilioni 16.1

Hasara ya mwaka huu ni kubwa ikilinganishwa na ile ya mwaka jana ya shilingi bilioni 12.2 huku shirika hilo likiendelea kukumbwa na misukosuko

Dismas Otuke
1 Min Read

Kampuni ya Ndege nchini Kenya Airways, imetanagza hasara ya shilingi bilioni 16.1, kutokana na ongezeko la bei ya mafuta iliyoongeza gharama ya kufanya biashara.

Hasara ya mwaka huu ni kubwa ikilinganishwa na ile ya mwaka jana ya shilingi bilioni 12.2 huku shirika hilo likiendelea kukumbwa na misukosuko

Kulingana na KQ bei ya mafuta ya ndege ilipanda kwa asilimia 66 kutokana na misukosuko ya kisiasa katika eneo la mashariki ya kati,hali iliyoongeza gharama ya mafuta ya ndege kwa asilimia 32.

KQ imesema kupanda kwa bei ya mafuta kulisukuma gharama ya kuendesha biashara kwa hadi asilimia 14.

Share This Article