Kenya na Ufaransa zashirikiana kuimarisha safari za ndege

Tom Mathinji
1 Min Read
Kenya na Ufaransa zashirikiana kuimarisha safari za ndege.

Shirika la Ndege Kenya Airways (KQ), limesema linaimarisha ushirikiano wake na Shirika la Air France la Ufaransa, kuboresha safari za ndege baina ya nchi hizo mbili.

Hayo yalisemwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa KQ George Kamal, aliposhiriki mkutano na balozi wa Ufaransa hapa nchini Arnaud Suquet katika Makao Makuu ya shirika hilo Jijini Nairobi.

“Mazungumzo yetu yaliangazia kuimarisha usafiri wa abiria kati ya Nairobi na Paris, ambao ni muhimu kwa biashara na Utalii kwa KQ na Shirika la Ndege la Air France,” alisema Kamal

Kulingana na Mkurugenzi huyo, mkutano huo pia uliangazia Kongamalo la Africa Forward litakalo andaliwa Jijini Nairobi mwezi Mei mwaka huu, ambalo ni la kwanza kabisa kuandaliwa katika nchi isiyozungumza Kifaransa.

“Tumejitolea kutekeleza jukumu letu la kubuni fursa mpya kwa bara hili na raia wake,” aliongeza Mkurugenzi huyo.

Share This Article