Timu ya taifa ya Kenya ,Harambee Stars itakuwa na klibarua kigumu itakaposhuka mjini Conakry leo Alhamisi jioni kwa mechi ya pili ya kundi D kufuzu kwa fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka ujao.
Kenya iliyo na alama moja pekee baada ya kwenda sare na Eritrea ,katika mechi ya kwanza wiki jana watajizatiti kusajili matokeo mazuri kama sehemu ya maandalizi kwa kipute cha AFCON ambacho wataandaa kwa pamoja na Tanzania na Uganda.
Afrika Kusini wanaongoza kundi hilo kwa alama sita baada ya kusajili ushindi wa mabao 5-0, dhidi ya Eritrea katika mechi ya jana.
Vijana wa Benny McCarthy walifanyza mazoezi ya mwisho jana jioni kujiandaa kwa mechi ya leo.