Boniface Ambani amechaguliwa Mwenyekiti mpya wa klabu ya AFC Leopards, baada ya kubuka mshindi wa uchaguzi wa Jumapili.
Mshambulizi huyo wa zamani wa Kenya na pia mchezaji wa zamani wa Leopards amezoa kura 1,101 dhidi ya mpinzani wake Vincent Enos Mutoka aliyepata kura 682.
Isaac Mulindi ndiye Katibu Mkuu kwa kupata kura 678 akifuatwa na Robert Situma aliyepata kura 534,huku Irene Sitawa akichukua nafasi ya tatu kwa kura 529 .
Newton Lime Luchacha amechaguliwa mweka hazina kwa kupata kura 676,akiwashinda Edwin Chamwada na Patrick Kanyangi waliopata kura 599 na 445 mtawalia.
Ambani anatwaa Uenyekiti kutoka kwa Dan Shikanda, ambaye amehudumu kwa mihula miwili.