Takriban wanajeshi wasiopungua 13 wa Niger waliuawa na wengine 20 kujeruhiwa katika shambulizi la kigaidi kwenye kambi yao eneo la Sanam, Tillabéri magharibi mwa Niger.
Kulingana na Wizara ya Ulinzi ya taifa hilo, shambulizi hilo lilitekelezwa siku ya Alhamisi na watu wasiojulikana.
Shambulizi hilo lilitokea alfajiri huko Sanam, karibu na mpaka wa Mali, eneo ambalo limekuwa likikumbwa na mashambulizi ya makundi yenye silaha.
Kwa mujibu wa taarifa iliyosomwa kwenye televisheni ya taifa, vikosi vya usalama vilisema viliwaua washambuliaji kadhaa, vikatibua miundombinu yao, na vinaendelea na operesheni ya kuwasaka waliohusika huku majeruhi wakipelekwa hospitalini.
Tukio hili limetokea siku mbili baada ya wanajeshi 11 wa Niger kuuawa katika shambulio linalohusishwa na kundi la Boko Haram huko Baroua, eneo la Diffa kusini-mashariki mwa nchi hiyo
Sio bayana ni nani alitekeleza shambulizi hilo.