Meli tatu za mafuta zateketezwa mlango wa bahari wa Hormuz

Maafisa wa usalama nchini Iran wa kundi la Revolutionary Guard, wamesema meli hizo zimelipuliwa na kuteketea katika eneo la Strait of Hormuz.

Dismas Otuke
1 Min Read

Meli tatu za  mafuta  zimeteketezwa mapema Jumapili katika mlango bahari wa Hormuz huku vita  kati ya Marekani na Iran vikichacha.

Inaaminika kuwa meli hizo zilikuwa baharini bila kibali ndiposa zikalipuliwa.

Maafisa wa usalama nchini Iran wa kundi la Revolutionary Guard, wamesema meli hizo zimelipuliwa na kuteketea katika eneo la Strait of Hormuz.

Aidha, wanaanga wa Saudi Arabia walidungua mabomu matatu yaliyolipuliwa na kundi la waasi waHouthi kutoka Yeman, na kusababisha kuporomoka kwa jumba la  orofa moja mjini Riyadh.

Kundi la Houthi limesa angaa watu 72 waliuawa kwenye mashambulizi ya angani katika mikoa minane ndani ya saa 48.

Share This Article