Afisa wa chama cha upinzani auawa Afrika Kusini

Maafisa wa Polisi Afrika Kusini wamesema kuwa visa 20 vya mauaji vinayowahusu wawakilishi, wanachama na wafuasi wa vyama vya kisiasa vimeripotiwa wiki iliyopita, wakati wa kipindi cha uchaguzi wa manispaa.

Tom Mathinji
1 Min Read
Afisa wa chama cha kisiasa auawa Afrika Kusini.

Mshirikishi wa chama kimoja cha upinzani ameuawa katika mkoa wa KwaZulu-Natal, Afrika Kusini na kuibua wasiwasi kuhusu kuibuka kwa ghasia za kisiasa kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa siku ya Jumatano.

Akithibitisha mauaji hayo, msemaji wa polisi Robert Netshiunda, alisema uchunguzi wa mauaji hayo umeanzishwa baada ya Lastborn Shazi wa chama cha uMkhonto weSizwe (MKP), kupigwa risasi nyumbani kwake alipokuwa kwenye mkutano kwa njia ya mtandao siku ya Jumatatu.

Maafisa wa Polisi Afrika Kusini wamesema kuwa visa 20 vya mauaji vinayowahusu wawakilishi, wanachama na wafuasi wa vyama vya kisiasa vimeripotiwa wiki iliyopita, wakati wa kipindi cha uchaguzi wa manispaa.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, ameagiza kupelekwa kwa maafisa wa jeshi zaidi ya 500 katika eneo la Kwazulu Natal, kupiga jeki vikosi vya polisi ambao wametambua vituo 165 vya kupiga kura kuwa kwenye hatari kubwa.

Siku ya Jumatano, wapigaji kura watawachagua madiwani, ambao watawachagua Meya watakaoongoza utoaji huduma kwenye manispaa ikiwa ni pamoja na huduma za maji, usafi na uzoaji wa taka.

Share This Article