Junior Harambee Starlets kukabiliana na Uchina Jumatatu,Kombe la Dunia

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya Kenya ya wanawake walio chini ya umri wa miaka 17-Junior Harambee Starletes, itamenyana na Uchina katika mchuano wa ufunguzi wa kundi E kuwania Kombe la Dunia Jumatatu jioni, katika uwanja wa Mohammed 6 mjini Rabat,Morocco.

Kenya inayofunzwa na Mildred Omari imekuwa nchini Morocco, tangu wiki jana ikijiandaa kushiriki Kombe la Dunia kwa mara ya pili baada ya kubanduliwa katika hatua ya makundi mwaka 2024 katika Jamhuri ya Dominica.

Junior Starlets watapambana na Uchina kuanzia saa kumi na mbili jioni kabla ya kukabiliana na Marekani Oktoba 22 na kukamilisha mechi za makundi dhidi ya Samoa siku tatu baadaye.

Share This Article