Kombe halisi la ligi Kuu nchini Uingereza liko nchini Kenya huku mashabiki shakiki wa ligi hiyo maarufu duniani wakipewa fursa ya kulitazama na kupiga nalo picha.
Siku ya Alhamisi kombe hilo la kifahari lililokabidhiwa klaby ya Arsenal msimu jana lilitua katika shirika la utangazaji nchini Kenya KBC.
Wanahabari wa KBC walipata fursa adimu ya kupiga picha kando yake.
Ziara hiyo inaandaliwa na kileo cha Guiness na kombe hilo liliwasilishwa Kenya Oktoba 13.
Mashabiki wa Kisumu watapata fursa ya kulitazama na kupiga nalo picha Ijumaa Oktoba 16, huku wale Nairobi wakijiburudisha na nalo siku ya Jumamosi Oktoba 17.