KRA yanasa rununu za iPhones za shilingi milioni 8.2 JKIA

Rununu hizo zilipatikana kutoka kwa abiria mmoja wa kiume aliyewasili kutoka Dubai mara nne ndani ya siku tisa.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru nchini Kenya (KRA) imenasa simu 40 za rununu aina ya iPhone 18 Pro na iPhone 18 pro max za thamani ya shilingi milioni 8.2.

Simu hizo zilinaswa na maafisa wa mamlaka hiyo katika Uwanja wa Ndege wa Kimayaifa wa Jomo Kenyatta, JKIA.

Rununu hizo zilipatikana kutoka kwa abiria mmoja wa kiume aliyewasili kutoka Dubai mara nne ndani ya siku tisa.

Wakati zikinaswa, zilikuwa zimepakiwa ndani ya begi tatu za kubebea mizigo na begi moja ya mgongoni.

Alipohojiwa, ilibanikika kuwa abiria huyo amekuwa akisafiri mara kadhaa akitumwa na mteja wake ambaye yuko Dubai na yamkini rununu hizo zilikusudiwa kuuzwa nchini Kenya.

Maafisa wa KRA walishuku safari nyingi za abiria huyo ndani ya muda mfupi za kutoka Kenya kwenda Dubai na kurejea humu nchini.

KRA imesisitiza kuwa itaendelea kutumia teknolojia ili kubaini mizigo inyoingizwa humu nchini kinyume cha sheria na kutoka kwa abiria wanaotaka kukwepa kulipa ushuru.

TAGGED:
Share This Article