Takriban watu 21 wamefariki kwenye ajali ya barabarani iliyohusisha magari kadhaa, Afrika Kusini.
Msemaji wa polisi Christopher Spies alithibitisha ajali hiyo ilitokea katika barabara kuu ya N1, na ilihusisha mabasi mawili madogo na gari aina ya Suzuki.
Spies alisema watu wanane walitangazwa kufariki papo hapo, watatu wakifariki walipokuwa wakipokea matibabu hospitalini, na kwamba watu wengine wanne walijeruhiwa kwenye ajali hiyo.
Kulingana na utawala nchini humo, ajali hiyo ni miongoni mwa ajali mbili kubwa zaidi kuripotiwa katika muda wa siku mbili zilizopita, ambapo watu wanane walifariki kwenye ajali katika mkoa wa Mpumalanga Jumapili asubuhi.
Idadi ya waliofariki huenda ikaongezeka, kulingana na maafisa wa kutoa huduma za dharura na wale wa utawala nchini humo.
Takwimu za Wizara ya Uchukuzi Afrika Kusini, zinadokeza kuwa watu 11,500 walifariki kwenye ajali za barabarani mwaka 2025.