Uganda imewashinda Senegal seti 3-0 katika mechi ya kundi B ,mashindano ya kuwania Kombe la mataifa ya Afrika iliyosakatwa katika uwanja wa Kasarani mapema Jumanne.
Uganda walisajili ushindi wa 25-21, 25-15 na 25-16, wakizoa jumla ya pointi 75, dhidi ya 52, huku mechi hiyo ikidumu kwa muda wa lisaa limoja na dakika 12.
Katika mchuano wa pili kundini B katika uwanja wa Kasarani, Misri imewacharaza Burkina Fasso seti 3-0 za 25-3,25-15, na 25-15.
Uwanjani Ulinzi, Rwanda imeikomoa Algeria seti bila jawabu za 25-22, 25-20 na 25-16, katika kundi D nao DR Congo, wakaititiga Burundi seti zizo hizo 3-0 pia katika ukumbi wa Ulinzi.
Mashindano hayo yanayoshirikisha mataifa 15 yatakamilika Septemba 5, huku mabingwa wakifuzu kushiriki mashindanio ya Dunia mwakani.