Rais William Ruto ametaka viongozi wa makanisa kuwa katika mstari wa mbele kuongoza mijadala ya kitaifa na kutoa muongozo kuhusu sera na ajenda za maendeleo ya taifa.
Akiwahutubia waumini wa kanisa la African Brotherhood Church (ABC) Women of Faith Congress katika chuo kikuu cha Machakos, siku ya Jumamosi,Rais alisema masuala muhimu ya taifa kama vile ruwaza ya mwaka 2030 yanapaswa kuwa kati ya masuala muhimu yanayoongozwa na kanisa.
Aliahidi kuendelea kushirikiana na kanisa la ABC katika kueneza injili humu nchini akiongeza kuwa atashirikiana nao kuhakikisha upanuzi wa chuo cha Eastern Kenya Integrated, ambacho maajuzi kimeidhinishwa kutoa mafunzo ya chuo kikuu nchini.
Awali Rais alizindua miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara ya Makaveti-Kyangala-Liyuni na kukagua ujenzi wa soko la Kimutwa kaunti ya Machakos.