Klabu ya Arsenal itafungua kampeni ya kutetea taji la ligi kuu Uingereza Ijumaa usiku itakapowaalika Coventry City waliopandishwa ngazi.
Arsenal walishinda taji hilo kwa mara ya kwanza Mei mwaka huu baada ya subira ya miaka 22, wakizoa pointi 82, kushinda mechi 25, kupiga sare saba na kupoteza tano.
Katika mechi nyingine za kufungua msimu Jumamosi, Hull City watawaalika Manchester United, Everton wakwangurane na Crystal Palace, Ipswich wakabane koo na Sunderland, Leeds United iwatembelee Nottingham Forest wakati Brentford wakifunga ratiba dhidi ya Tottenham katika Derby ya London.
Jumapili, Aston Villa watakutana na Brighton, Manchester City wawe nyumbani kupimana nguvu na Bournemouth, kisha Liverpool wafunge wikendi dhidi ya Newcastle United.
Fulham watakamilisha raundi ya kwanza kwa kuwaalika Chelsea Jumatatu usiku.