Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC inatarajiwa kupokea dozi 70,000 za chanjo ya Everbo kutoka kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) ili kudhibiti maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Ebola.
DRC iliitisha dozi hizo wiki jana huku WHO ikisema chanjo 20,000 kati ya hizo zitatumika kutathmini athari yake kwa wagonjwa ambao wamekaa na virusi vya Ebola kwa kipindi kirefu.
Chanjo ya Everbo imethibitishwa kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya Bundibugyo, vinavyosababisha ugonjwa wa Ebola.
Haya yanajiri wakati ambapo zaidi ya visa 5,000 vya Ebola vimeripotiwa nchini DRC .