Uteuzi wa wagombeaji Urais kukamilika Mei 24, yasema IEBC

IEBC imepanga kuendesha uchaguzi mkuu wa mwaka ujao utakaoandaliwa Agosti 10.

Dismas Otuke
1 Min Read
Erastus Ethekon - Mwenyekiti wa IEBC

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, IEBC imetangaza Mei 24 mwaka ujao kuwa siku ya mwisho ya uteuzi wa wagombeaji Urais kwa uchaguzi mkuu.

Kwenya arifa yake ya Alhamisi jioni, IEBC ilisema kila mwaniaji Urais ni sharti awasilishe orodhha ya watu 2,000 wanaomuunga mkono na kutimiza masharti mengine muhimu kwa mjibu wa sheria.

Baada ya kufungwa kwa uwasilishaji karatasi za uteuzi kwa waaniaji Urais, IEBC itaanza kuwapiga msasa wagombeaji wote kati ya Mei 29 na Juni Juni 11.

IEBC imepanga kuendesha uchaguzi mkuu wa mwaka ujao utaandaliwa Agosti 10.

Share This Article