Kiongozi wa upinzani nchini Zambia Brian Mandubile amepinga matokeo ya urais katika uchaguzi mkuu wa wiki jana huku akiapa kuwasilisha kesi mahakamani.
Mandubile amesema kulikuwa na udanganyifu mwingi katika uchaguzi huo na kuongeza kuwa haukuwa huru na wa haki.
Kiongozi huyo wa chama cha National Reconciliation Party for Unity and Prosperity (NRPUP) amesema kampeni zao zilighubikwa na kuingiliwa pakubwa na serikali huku pia mchakato wa ujumuishaji kura na kutangaza matokeo ukiwa na kasoro nyingi.
Wachunguzi wa uchaguzi huo kutoka Umoja wa Ulaya pia wametilia shaka matokeo ya uchaguzi huo wakisema haukuwa huru.
Tume ya Uchaguzi nchini Zambia ilimtangaza Rais Hakainde Hichelema kuwa mshindi wa uchaguzi huo kwa kuzoa asilimia 60 huku Mandubile akifuata kwa umbali kwa asilimia 38.