Watu zaidi ya 40 wafariki kwenye ajali ya feri Zimbabwe

Idara ya Polisi ilisema ajali hiyo ilitokea baada ya feri hiyo kupigwa na mawimbi makali, huku shughuli za utafutaji na uokoaji zikiendelea.

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu zaidi ya 40 wafariki baada ya feri kuzama nchini Zimbabwe.

Abiria zaidi ya 40 wamefariki na wengine kadhaa hawajulikani waliko baada ya feri walimokuwa wakisafiria kuzama katika Ziwa Kariba nchini Zimbawe.

Kulingana na mamlaka nchini humo, feri hiyo ilikuwa na abiria 114, wahudumu watano licha ya kwamba ilikuwa na uwezo wa kuwabeba watu 90.

Idara ya Polisi ilisema ajali hiyo ilitokea baada ya feri hiyo kupigwa na mawimbi makali, huku shughuli za utafutaji na uokoaji zikiendelea.

Hadi kufikia wakati wa kuchapisha taarifa hii, watu77 walikuwa wameokolewa. Idadi isiyojulikana ya watoto wanaaminika walikuwa kwenye feri hiyo, ajali hiyo ilipotokea.

Feri hiyo huwasafirisha watu kati ya mji wa Kariba, visiwa vingne na vijiji vya wavuvi

Ajali hiyo ndio mbaya zaidi kuwahi nakiliwa katika ziwa hilo, ambalo liko kwenye mpaka na Zambia na zaidi ya kilomita 300 kutoka Jiji Kuu Harare.

Share This Article