Yanga yamsajili Selemani Mwalimu

Alitambulishwa Jumamosi Agosti 8 2026, kuwa mchezaji wa mkopo kwa msimu huu wa 2026/27 kwenye Simba Day, na sasa mambo yamebadilika.

Marion Bosire
1 Min Read

Timu ya soka nchini Tanzania Yanga SC imetangaza kwamba imekamilisha usajili wa aliyekuwa mshambuliaji wa timu ya Wydad Casablanca ya Morocco Selemani Mwalimu.

Msimu uliopita mchezaji huyo alikuwa akiichezea Simba SC kwa mkopo kutoka Wydad, huku timu hiyo ikimtambulisha kwa msimu huu wa 2026/27 Jumamosi ya Agosti 8 2026 kwenye Simba Day.

Simba SC ambao ni mahasimu wa Yanga walitangaza Jumamosi kwamba Selemani Mwalimu almaarufu “Gomez” angeendelea kubaki huko kwa mkopo wa msimu mzima wa 2026/27 kutoka Wydad Casablanca.

Hata hivyo, katika mabadiliko ya kushangaza, wapinzani wao wakuu Young Africans au Yanga SC walifanikiwa kunyakua fursa hiyo haraka na kumtambulisha rasmi baada ya kukamilisha makubaliano na Wydad.

Agosti 4, 2026, afisa wa habari wa Yanga SC Ally Kamwe alisikika akisema kwamba Simba walikuwa wakifanya nae mazoezi lakini ni mchezaji wao na wakati huo Mwalimu alikuwa Kigali Rwanda na Simba SC wakijiandaa na msimu mpya.

Share This Article