Iran: Mohsen Rezaei ateuliwa kiongozi mpya wa Baraza Kuu la Usalama

Rezaei anachukuwa nafasi ya Bagher Zolghadr, ambaye alishikilia wadhifa huo kwa muda wa miezi michache, baada ya mtangulizi wake Ali Larijani, kuuawa kwenye shambulizi la ndege mwezi Machi.

Tom Mathinji
1 Min Read
Mohsen Rezaei, ateuliwa kiongozi mpya wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran.

Mohsen Rezaei, ameteuliwa kuwa kiongozi mpya wa Baraza la Kuu la Usalama la Iran kwenye tangazo lililotolewa Jumapili na kiongozi wa taifa hilo Mojtaba Khamenei.

“Kutokana na tajiriba yako, ninakuteuwa kuwa mwakilishi wangu kwenye Baraza Kuu la Usalama wa Taifa,” alisema Khamenei akimtaja Rezaei kuwa mkongwe wa vita vya mwaka 1980–1988 kati ya Iran na Iraq.

Rezaei anachukuwa nafasi ya Bagher Zolghadr, ambaye alishikilia wadhifa huo kwa muda wa miezi michache, baada ya mtangulizi wake Ali Larijani, kuuawa kwenye shambulizi la ndege mwezi Machi.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 71, mwezi Julai alisema kuwa kudhibiti mlango bahari wa Hormuz ni muhimu sana kuliko kumiliki mabomu ya atomiki.

Huku akishikilia wadhifa huo, Rezaei sasa atakuwa mshauri wa kisiasa wa Khamenei, wakati huu ambapo Iran inaendelea kukabiliana na Marekani hususan kuhusu kufunguliwa kwa mlango bahari wa Hormuz.

Share This Article