Mfaransa Herve Renard ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tunisia -Carthage Eagles, kutwaa nafasi ya Sabri Lamouchi, aliyepigwa kalamu Jumatatu kufuatia kichapo cha 5-1, na Uswidi.
Lamouchi,ambaye aliteuliwa Januari mwaka huu kuingoza Tunisia, alikuwa amesaini mkataba na Carthage Eagles,na ndiye mkufunzi wa kwanza kupigwa teke katika fainali za Kombe la Dunia mwaka huu.
Renard aliye na umri wa miaka 57 alishinda kombe la AFCON na timu za Zambia, mwaka 2012 na Ivory Coast mwaka 2015.
Mfaransa huyo alikuwa kocha mkuu wa Morocco katika Kombe la Dunia mwaka 2018,wakifuzu baada ya kuwa nje kwa miaka 20.
Kibarua cha kwanza kwa Renard itakuwa ni mechi ya pili ya kombe la Dunia dhidi ya Japan Juni 20, kabla ya kuhitimisha ratiba na Uholanzi siku tano baadaye.