Blue Samurai ya Japani ilitoka nyuma mara mbili na kunusuru alama katika sare ya 2-2 dhidi ya Wanachungwa kutok Uholanzi mjini Dallas katika kundi E, mechi iliyotitigwa uwanjani Dallas nchini Mareani Jumapili usiku.
Baada ya timu zote kuambulia sare tasa katika dakika 45 za kwanza, nahodha wa Uholanzi Virgil van Dijk alipachika bao la ufunguzi kwa Uholanzi dakika sita baada ya kipindi cha pili kuanza.
Blue Samurai ya Japani walisawazisha dakika sita na baadaye Crysencio Summerville, akairejesha Uholanzi uongozini huku magoli yote ya Waholanzi yakichangiwa na Ryan Gravenberch.
Kiungo wa Crystal Palace Daichi Kamada naye alihakikisha Japani wanazoa alama hiyo moja muhimu alipofyatua tobwe na kutua kimiani dakika mbili kabla ya kipenga cha mwisho.