Serikali yawekeza shilingi bilioni 15.6 kwa nyumba za bei nafuu Wajir

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto.

Rais William Ruto amesema serikali imewekeza shilingi bilioni 15.6, kwa ujenzi wa nyumba 4,600 za gharama nafuu katika kaunti ya Wajir.

“Huu ndio mradi mkubwa zaidi wa ujenzi wa nyumba kuwahi shuhudiwa katika kaunti ya Wajiri tangu nchi hii ilipopata uhuru,” alisema Rais Ruto.

Rais Ruto alisema ujenzi wa nyumba hizo za bei nafuu ni ishara ya kujitolea kwa serikali  kuhakikisha maendeleo, upatikanaji wa fursa na kuishi kwa mazingira safi na kwamba hazijatengewa watu wa baadhi tu ya maeneo.

“Miradi hii inabuni nafasi za ajira kwa vijana na kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa maeneo ya mashinani,’ alidokeza kiongozi huyo wa taifa.

Akihutubia taifa leo Jumatatu wakati wa sherehe za 63 katika kaunti ya Wajir, Rais Ruto alisema mradi wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu katika kaunti za Wajir, Garissa, na Mandera, utagharimu shilingi bilioni 38.5.

“Uwekezaji huu unafanikisha upatikanaji wa nyumba za bei nafuu, nyumba za malazi za wanafunzi, masoko ya kisasa, nyumba za maafisa wa polisi, madarasa na miundombinu mingine ambayo inachochea maendeleo,” alidokeza Rais Ruto.

Ni mara ya kwanza kwa sherehe hizo kuandaliwa katika kaunti ya Wajir.

Share This Article