Timu ya Kenya ya wanawake wasiozidi umri wa miaka 17, itawaalika Uganda, katika marudio ya raundi ya pili kufuzu fainali za Kombe la Dunia leo Jumamosi.
Pambao hilo litapigwa uwanjani Nyayo kuanzia saa tisa, huku mshindi wa jumla akijikatia tiketi kwa raundi ya tatu na ya mwisho.
Kenya na Uganda zilitoka sare ya bao moja katika duru ya kwanza wiki jana mjini Kampala.
Junior Starlets ya Kenya chini ya kocha Mildred Cheche, inalenga kufuzu kwa mara ya pili kwa Kombe la Dunia baada ya kushiriki fainali za mwaka 2024, katika Jamhuri ya Dominika.
Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu kwa wanawake wasiozidi umri wa miaka 17, zitaandaliwa kati ya Oktoba 17 na Novemba 7 nchini Morocco.