Samia na Bunge la Tanzania wapongeza Serengeti Boys kufuzu Kombe la Dunia

Tanzania itashuka uwanjani Rabat Juni 2 kwenye fainali dhidi ya Senegal.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais Samia Suluhu ameipongeza timu ya taifa ya soka ya wanaume chini ya umri wa miaka 17, baada ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza.

Serengeti Boys pia ilifuzu kwa fainali ya mashindano ya AFCON, yanayoendelea nchini Morocco, baada ya kuwashinda Misri penati 4-3, baada ya sare tasa  katika nusu fainali .

Rais Samia ameyataja mafanikio hayo kuwa ni hatua muhimu kwa maendeleo ya soka la vijana nchini na yanaakisi vipaji, juhudi na nidhamu ya vijana wa Tanzania katika uwakilishi wa nchi kwenye mashindano ya kimataifa.

Aidha Bunge la Tanzania limeongoza mjadala siku ya Ijumaa kuipongeza timu hiyo kufuatia matokeo hayo bora.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amesema uwekezaji huo umezaa matunda .
Akichangia azimio la Bunge la kuipongeza Serengeti Boys, Makonda amesema wizara yake itaendelea kuwalea vijana hao kwa ajili ya mashindano ya AFCON ya mwaka 2030.
Tanzania itashuka uwanjani Rabat Juni 2 kwenye fainali dhidi ya Senegal.

 

Share This Article