Mshukiwa wa uhalifu akamatwa na sare za jeshi Nairobi

Tom Mathinji
1 Min Read
Mshukiwa wa uhalifu akamatwa na sare za KDF Nairobi.

Maafisa wa usalama wamemkamata mshukiwa wa uhalifu akiwa na risasi moja na sare za maafisa wa jeshi la Ulinzi la Kenya (KDF).

Baada ya kupokea habari za kijasusi, maafisa hao walifanya msako uliosababisha kukakamtwa kwa Rodgers Omondo Odhiambo ambaye ni afisa wa zamani wa KDF nyumbani kwake mtaa wa Kayole.

Kupitia ukurasa wa X, Maafisa wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), imesema mshukiwa huyo aliwapeleka maafisa hao katika makazi yake ambapo walipata sare na vifaa vingine vya vinavyotumiwa na jeshi la ulinzi la Kenya

Baadaye alifikishwa kwenye mahakama za milimani ambako alifunguliwa mashtaka ya kumiliki risasi na sare za jeshi kinyume cha sheria.

Aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja, huku kesi hiyo ikitarajiwa kutajwa Juni 2, 2026.

TAGGED:
Share This Article