Bilionea wa Tanzania Mohammed Dewji, ametangaza kuekeza dola za Kimarekani milioni 50, sawa na shilingi bilioni 6.4 za kenya, kwa ujenzi wa kiwanda cha kutengeza soda katika kaunti ya Mombasa.
Kampuni ya MeTL Group, inayomilikiwa na Dewji, inatarajia kupanua biashara yake hadi Kenya, kwa kutengeza bidhaa za soda kama vile Mo Cola,Mo Extra na Mo Malto.
Ili kutoa ushindani mkali kwa kampuni za Pepsico na Coca Cola,MeTL inapania kuuza soda zake za milimita 300 kwa shilingi 15 ,shilingi 25 chini ya wapinzani wake sokoni.
Kulingana na jarida la Citizen nchini Tanzania, mipango inaendelea huku ujenzi wa kiwanda hicho ukitarajiwa kuanza mapema mwaka ujao.