Rais wa shirikisho la soka barani Afrika (CAF) ,Dkt Patrice Motsepe, atahudhuria na kuzungumza kwenye kongamano la Africa Forward jijini Nairobi, siku ya Jumatatu..
Kongamano hilo litaandaliwa kati ya Jumatatu na Jumane Mei 11 na 12.
Kenya ni mojawapo wa waandalizi watatu wa fainali za 36, za kombe la mataifa ya Afrika mwaka ujao baina ya Juni na Julai.
Akiwa Nairobi, Motsepe, atafanya mkutano na maafisa wakuu wa serikali za Kenya,Uganda na Tanzania, kuhusiana na maandalizi ya kipute cha AFCON mwaka ujao.