Wakenya Sawe,Obiri na Jepkosgei kushiriki London Marathon leo

Dismas Otuke
1 Min Read

Mkenya Mathew Sawe atajitosa uwanjani leo Jumapili kutetea taji ya mbio za London Marathon  nchini Uingereza.

Sawe atakabiliana na upinzani mkali kutoka kwa Waganda Joshua Cheptegei na Jacob Kiplimo, na wanariadha kutoka Ethiopia Tamirat Tola, na  Yomif Kejelcha.

Mbio za wanaume zinatazamiwa kuanza saa tano na dakika 35 leo asubuhi, ikiwa nusu saa baada ya wanawake kuanza.

Mbio za wanawake zitawashirikisha Wakenya Hellen Obiri na Joyceline Jepkosgei, watakaopambana  na bingwa mtetezi Tigst Assefa.

Mbio za London zitakuwa za tatu katika msururu wa mbio kuu Ulimwenguni, baada ya Tokyo Marathon mwezi jana na Boston Marathon Jumatatu wiki hii.

Share This Article