Katibu wa usalama wa kitaifa Raymond Omollo amewaonya wanasiasa dhidi ya kuwatumia vijana vibaya katika kaunti ya Kisumu.
Omollo amesema haya siku ya Jumamosi alipokutana na viongozi wa Wanabodaboda kutoka maeneo bunge saba ya kaunti ya Kisumu ikiwemo Kisumu East, Kisumu West, Kisumu Central,
Seme, Nyando, Nyakach, na Muhoroni.
Kikao hicho kilitumika kwa vijana hao wa Bodaboda kusema yanayowasibu na jinsi ambayo serikali itawapiga jeki kujiinua kimaisha.
Omollo alionya kuwa serikali haitaruhusu visa vyovyote vya utovu wa usalama katika mikutano ya kisiasa na kuwataka wakenya kuheshimu uhuru wa kila mmoja kujieleza bila kuzua vurugu.