Shakib adai kwamba marafiki wa Zari hawawatakii mema

Anasema marafiki wa Zari wamekuwa wakikosoa ndoa yao huku wakitaka ivunjike

Marion Bosire
2 Min Read

Shakib Cham ambaye ni mwanasoshiolaiti na mfanyibiashara wa Uganda amefichua mazito kuhusiana na yanayosibu ndoa yake na mwanasoshiolaiti na mnfanyibiashara Zari Hassan.

Cham ambaye amekuwa kwenye ndoa na Zari tangu Oktoba 2023 anasema kwamba ndoa yao imekuwa ikikabiliwa na jicho baya kutoka kwa marafiki wa Zari.

Ndoa ya Zari and Shakib haijakuwa bila matatzo na misukosuko lakini wawili hao wameweza kusalia imara.

Shakib anasema marafiki wa Zari wamekuwa wakikosoa ndoa yao huku wakitaka ivunjike lakini katika mahojiano, alisema kwamba ndoa yao inaendelea kuwa imara na kwamba haitavunjika hadi mwenyezi Mungu aridhie.

Cham sasa anawataka wakosoaji wa ndoa yao wakome kujaribu kuwatenganisha kwani hawawezi kuvunja alichounganisha Mungu.

“Marafiki wa mke wangu wanaiwinda sana ndoa yetu. Baadhi ya marafiki zake ndio wakosoaji wetu wakuu, lakini niko hapa kuwaambia kwamba haitaisha hadi Mungu ambaye aliitengeneza aamue kuimaliza,” alisema Cham kwenye mahojiano hayo.

Haya yanajiri wiki kadhaa tangu wakati Zari alionya wanablogu waliosambaza taarifa za uwongo kwamba ndoa yake na Shakib inakumbwa na matatizo na huenda imevunjika.

Picha za kile kilichoonekana kuwa chapisho la Zari mitandaoni ambapo alikuwa analalamikia hatua ya Shakib ya kukosa kuwa mwaminifu kwa ndoa yao.

Zari alifafanua kwamba picha hizo sio za ukweli bali ni za kugushi na kamwe hakuchapisha habari hizo.

Share This Article