Rais William Ruto Jumapili jioni ameanzisha ujenzi wa uwanja wa michezo wa Gusii kwa gharama ya shilingi bilioni 1.
Akiwahutubia wananchi katika uwanja wa Gusii baada ya kuweka jiwe la msingi ,Rais ameongeza kuwa atatoa shilingi milioni 20 kugharamia malipo ya uwanja mbadala utakaotumika na klabu hiyo katika kipindi cha miezi tisa ya ujenzi wa uwanja huo.
Punde utakapokamilika uwanja huo utamudu mashabiki 14,000 na utatumiwa na klabu ya Shabana FC inayoshiriki Ligi Kuu.
Rais ameanza ziara yake ya siku nne katika eneo la Kisii anapotrajiwa kuanzisha miradi kadhaa ya maendeleo.
Jumatatu Rais atazuru kaunti za Nyamira na Kisii kukagua na kuanzisha miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara,na ujenzi wa uwanja wa ndege wa Suneka miongoni mwa miradi mingine.