Vijana wahimizwa kulinda ukweli kuhusu mauaji ya halaiki nchini Rwanda

Waziri wa masuala ya vijana na sanaa Sandrine Umutoni anahimiza vijana kuchukulia hostoria ya mauaji ya halaiki kama jukumu lao na kuzuia upotoshaji.

Marion Bosire
2 Min Read
Sandrine Umutoni, Waziri wa masuala ya vijana na sanaa nchini Rwanda.

Vijana nchini Rwanda, wamehimizwa kulinda ukweli kuhusiana na mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 yaliyolenga wa Tutsi.

Wito huu ulitolewa na waziri wa masuala ya vijana na sanaa Sandrine Umutoni, aliyesisitiza kwamba kumbukumbu ni muhimu katika kuunda mustakabali wenye umoja na ufahamu.

Alisema haya Ijumaa Aprili 10, 2026, katika awamu ya kwanza ya “Cine Kwibuka” jukwaa jipya la sinema linalolenga kuhakikisha kumbukumbu kupitia filamu.

Hafla hiyo iliandaliwa huko Canal Olympia Rebero, na ilihusisha maonyesho ya filamu mbili za matukio halisi ambazo ni “Reclaiming History – Colonial Roots of the Genocide in Rwanda” iliyoandaliwa na Samuel Ishimwe wa asili ya Rwanda na Matthias Frickel.

Nyingine ni “Things We Don’t Say” iliyoandaliwa na Ornella Mutoni wa asili ya Rwanda anayeishi jijini London, nchini Uingereza.

Waziri Umutoni alisisitiza kwamba kipindi cha Kwibuka ni muhimu katika kukumbuka wahasiriwa, kusimama na walionusurika na kuangazia jukumu la pamoja la kitaifa.

Filamu hizo mbili alisema zinaangazia masuala mawili ya ukweli kwamba mizizi ya mauaji ya halaiki ilikuwa katika historia ya muda mrefu ya migawanyiko na upotoshaji na pili athari zake zinahisiwa na vizazi kadhaa.

Huku akikiri kuhusu jukumu muhimu la filamu kama chombo cha simulizi, kama daraja kati ya vizazi, nafasi ya majadiliano na chombo cha kulinda kumbukumbu na ubinadamu, waziri Umutoni aliwataka vijana kuchukulia hstoria kama jukumu.

Share This Article