Katibu wa Wizara ya afya Mary Muthoni siku ya Jumamosi aliongoza shughuli ya kuwahamasisha wakazi wa kaunti ndogo ya Gichugu kaunti ya Kirinyaga kusajili na bima mpya ya matibabu ya SHA chini ya mpango wa Jamii Imara Mashinani .
Muthoni alielezea mafao ya SHA kwa wananchi akisisitiza kuwa itafanikisha juhudi za serikali za kupata huduma bora za matibabu kwa bei nafuu kwa wote nchini.
Aidha alijadiliana na wananchi kuhusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali katika eneo hilo ikiwemo ujenzi wa nyumba za gharama nafuu,ujenzi wa masoko ya kisasa,ujenzi wa miundo mbinu ya barabara,miradi ya unyunyuziaji maji mashamba inayolenga kuboresha kilimo.