IEBC imewasajili wapiga kura wapya 875,501

Tom Mathinji
1 Min Read
IEBC yasitisha usajili endelevu wa wapiga kura Eneo Bunge la Ol Kalou.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), imewasajili wapiga kura wapya  875,501 tangu Macho 30,2026.

Kulingana na IEBC, idadi imeongezeka na wapiga kura 531,185 tangu Aprili 3, 2026 hadi sasa.

Kupitia ukurasa wa X, IEBC iliwashukuru wakenya kwa kujitokeza kwa wingi wakati huu wa kipindi cha usajili endelevu wa wapiga kura.

Tume hiyo ilisema wapiga kura 49,502, wamehama kutoka vituo vyao vya kupigia kura hadi vingine, huku wapiga kura 1,066 wakibadilisha maelezo yao.

IEBC ilisema usajili endelevu wa wapiga kura unaendelea kila siku hadi mwishoni mwa wiki na Siku Kuu za umma.

Tume hiyo ilizindua usajili endelevu wa wapiga kura Macho 30,2026, kujiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2027

TAGGED:
Share This Article