Washukiwa watatu wakamatwa na lita 18,000 za Ethanol Busia

Huduma ya Taifa ya Polisi ilisema maafisa hao walipata mitungi 76 ya plastiki, kila moja ikiwa ya lita 250.

Tom Mathinji
1 Min Read
Polisi wanasa lita 18,000 za Ethanol Busia.

Maafisa kutoka asasi mbali mbali za usalama katika kaunti ya Busia , wamenasa lita 18,500 za ethanol zilizokuwa zikisafirishwa katika barabara ya Amase- Amongura.

Maafisa hao walisimamisha lori ambalo lilitiliwa shaka, na baada ya kulipekua walipata bidhaa hiyo bila stakabadhi rasmi.

Kupitia ukurasa wa X leo Ijumaa, Huduma ya Taifa ya Polisi ilisema maafisa hao walipata mitungi 76 ya plastiki, kila moja ikiwa ya lita 250.

“Kiasi cha Ethano kilichonaswa ni lita 18,500,kinachokadiriwa kuwa cha shilingi 22,200,000,” ilisema Huduma ya Taifa ya Polisi.

Kulingana na huduma hiyo, washukiwa watatu walikamatwa na wanazuiliwa wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Lori hilo linazuiliwa katika kituo cha polisi cha Adungosi, huku uchunguzi ukiendelea.

TAGGED:
Share This Article